Mungu Aliyeumba Kila Kitu Duniani

Wakati mwingine watu huuliza maswali kama, “Ulimwengu huu uliumbwaje?” na “Mwanadamu alitoka wapi, na anakwenda wapi?” Shule za leo hufundisha nadharia ya mageuzi ya Darwin pekee, hivyo watu wengi wameamini kwamba ulimwengu ulitokea kwa bahati na viumbe hai vimeendelea kubadilika hadi leo.

Kwa hiyo, wanakataa kwamba Mungu aliumba ulimwengu na kila kitu kilichomo, na wanashindwa kutambua kwamba mbingu na jehanamu vipo. Hutafuta tu anasa za duniani na mwishowe huishi maisha yao bure. Hata Charles Darwin, mwanzilishi wa nadharia ya mageuzi ya Darwin, alikiri kwamba Mungu ndiye Muumba Mkuu. Rafiki zake wengi walipomtembelea muda mfupi kabla ya kifo chake, aliwaambia, “Nimekuwa mpumbavu. Nimekuwa na mashaka juu ya kila kitu na kila aina ya matukio. Nadharia ya mageuzi ni mojawapo ya hayo.”

Kwa bahati mbaya, watu wengi waliishikilia nadharia hiyo kwa bidii kana kwamba ni dini yao na wakakataa uumbaji wa Mungu. Ningependa kuwaomba mshuhudie uumbaji mkuu wa Mungu na neema ya ukombozi wa Yesu Kristo. Nyumba tunazoishi hazikujengwa tu kwa bahati. Mtu alizibuni na kuzijenga. Vivyo hivyo, Mungu wa pekee wa kweli ndiye aliyebuni na kuumba ulimwengu na kila kitu kilichomo.

Kitabu cha Mwanzo kinaeleza wazi uumbaji wa mbingu, nchi na kila kitu kilichomo. Mwanzo 1:1 inasema, “Mungu aliziumba mbingu na nchi,” na Mwanzo 2:7 inasema, “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”

Kila kabila na jamii ina macho mawili, masikio mawili, pua moja yenye matundu mawili na mdomo mmoja. Muundo wa uso wa kila mwanadamu unafanana kikamilifu. Mtu anaweza kuuliza, “Wote wanafanana kwa sababu ni wanadamu.” Lakini hili linatuonyesha kwamba watu wote wametokana na mwanamume mmoja na mwanamke mmoja. Tunatambua kwamba mwanamume na mwanamke wa kwanza waliumbwa na Mungu Muumba mmoja. Kama kungekuwa na waumbaji wengi, baadhi ya watu wangekuwa na macho kadhaa na miundo ya nyuso ingetofautiana kulingana na mipango ya kila muumba. Zaidi ya hayo, tunaweza kutambua mguso wa Mungu kupitia matukio mbalimbali ya asili.

Kwa mfano, mvuto wa mwezi husababisha kupwa na kujaa kwa maji na kuyafanya maji ya bahari yasogee na kujisafisha. Upepo huvuma, maji huvukiza, mawingu hutokea na kusonga, kisha mvua hunyesha ardhini. Mambo hayo yote ni muhimu kwa uhai wa viumbe vyote. Hata ukweli huu mmoja unapaswa kutuwezesha kuamini kikamilifu kwamba Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na kila kitu kilichomo.

Nawasihi kila mmoja wenu aamini kwamba Mungu ndiye Muumba, yu hai hata sasa na anatawala kila kitu. Yeye peke yake ndiye anayetawala uzima na kifo, mafanikio na misiba ya wanadamu. Mtiini kama Abrahamu alivyofanya, mpate wokovu na uzima wa milele, na mfurahie baraka duniani. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu!

    His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee

Word of Life