Katika 2 Mambo ya Nyakati sura ya 20, jeshi kubwa la Wamoabu na Waamoni lilipovamia, Mfalme Yehoshafati aliwashinda kabisa maadui kwa kumtegemea Mungu peke yake.
Unabii wa nabii wa Mungu ulisema kwamba wangeshinda jeshi lililokuwa likivamia. Yehoshafati aliliamini Neno hilo, akawateua watu waliokuwa wamevaa mavazi matakatifu wamsifu Mungu na kuwatuma waende mbele ya jeshi wakiimba sifa. Kisha maadui wakapigana wao kwa wao na kuangamizana kabisa. Zaidi ya hayo, Mfalme Yehoshafati alipata nyara nyingi za vita.
Vivyo hivyo, hakuna jambo lisilowezekana kwako ukimtegemea Mungu Mwenyezi. Mithali 21:31 inasema, “Farasi huandaliwa kwa siku ya vita; lakini ushindi hutoka kwa Bwana.” Ukimkabidhi Mungu kila jambo—vita, familia, kazi na biashara—unaweza kuishi maisha ya ushindi daima. Siri za kuishi maisha ya ushindi katika hali yoyote ni zipi?
Kwanza, mtegemee Mungu kwa unyenyekevu katika kila jambo. Hata uwe na hekima na uwezo kiasi gani, unapaswa kwanza kuomba na kuchunguza mapenzi ya Mungu.
Pili, lisikilize na ulifuate mwongozo na uongozi wa Roho Mtakatifu. Hata kama umekuwa Mkristo kwa muda mrefu na una maarifa mengi ya Biblia, huwezi kuongozwa na Roho Mtakatifu bila kutahiriwa kwa moyo. Kadiri unavyoondoa dhambi na kuutakasa moyo wako, ndivyo utakavyoweza kusikia sauti yake na kuongozwa na kutawaliwa naye kwa uwazi zaidi; ndipo pia utaweza kuelewa na kutenda kwa hekima ya Mungu.
Tatu, tii kikamilifu sauti ya Roho Mtakatifu. Usipoitii sauti yake, hawezi tena kutenda kupitia kwako. Jambo baya zaidi ni kwamba ukiendelea kutotii, sauti yake itazidi kufifia naye atasita kuongoza maisha yako.
Hatimaye, ataacha kukuongoza. Kwa hiyo, ukitambua mapenzi ya Mungu kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, daima uwe tayari kutii hata kama jambo hilo halionekani kuwa na faida kwako au linakuweka katika hali ngumu. Mithali 16:3 inasema, “Mkabidhi Bwana kazi zako, nayo mawazo yako yatathibitika.” Watu wa ulimwengu hutegemea bure hekima, maarifa na nguvu zao wenyewe. Lakini hakuna lisilowezekana kwa watoto wa Mungu wanaoamini kwamba Mungu yu hai na kumkabidhi matatizo yao kabisa.
Ninaomba kila mmoja wenu amtegemee kikamilifu Bwana wa majeshi katika kila jambo analofanya na aishi maisha ya ushindi. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu!
His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee
Abrahamu, baba wa imani, aliitwa “rafiki wa Mungu.” Alikuwa mwanadamu wa kawaida, lakini alistahili kuitwa rafiki wa Mungu. Hili linathibitisha jinsi alivyomfanana Mungu kwa ukamilifu.
Mfalme na maafisa wake walimwacha Mungu na kuabudu sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikawajia watu wa Yuda, nao wakavamiwa na jeshi la Waaramu.
Roho Mtakatifu ni zawadi ya Mungu kwa watoto wake na ni hakikisho kwamba sisi ni watoto wa Mungu. Matendo 2:38 inasema: “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu;”