Ninaomba maisha yenu yajazwe upendo na baraka za Mungu. Sasa ningependa kushiriki nanyi neema kupitia ujumbe wenye kichwa “Wema wa Kutafuta Njia Ipasayo.”
Njia ipasayo inamaanisha mambo ambayo wanadamu wanapaswa kutimiza. Watoto wanapaswa kuwahudumia wazazi wao, ndugu wanapaswa kupendana, na walio wadogo wanapaswa kuwaheshimu walio wakubwa. Watu wanapofuata njia inayowapasa, tunaweza kusema wanatimiza wajibu wao kama wanadamu.
Ruthu, anayetajwa katika Agano la Kale, ni mmoja wa watu waliofuata njia ipasayo na kupokea baraka. Alikuwa mwanamke Mmoabu aliyeolewa na mwanamume Mwebrania aliyehamia Moabu kwa sababu ya njaa. Lakini wanaume wote wa familia hiyo walikufa bila kuacha wazao. Waliosalia walikuwa Naomi na wakwe zake wawili, Orpa na Ruthu. Naomi aliposikia kwamba mavuno yalikuwa mengi Bethlehemu ya Yuda, aliamua kurudi nyumbani kwake.
Akawaambia wakwe zake warudi nyumbani kwao na kuishi kwa amani katika nyumba zao. Orpa alilia, akambusu Naomi na kurudi nyumbani kwake kwa kusita. Lakini Ruthu hakurudi. Katika Ruthu 1:16 alisema, “Usinisihi nikuache, nirudi nisifuatane nawe; maana wewe uendako nitakwenda, nawe ukaapo nitakaa; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.” Azimio lake la kutimiza wajibu wake kama mwanadamu halikubadilika, naye akamfuata mama mkwe wake hadi nchi ya Yuda asiyoijua.
Ruthu alifuata njia ipasayo hata kwa kujitoa mwenyewe. Kama angerudi nyumbani kwa mama yake, angeishi maisha ya amani pamoja na familia na jamaa zake. Lakini alichagua kumhudumia mama mkwe wake. Chaguo hilo linaweza kuonekana kama hasara, lakini Mungu anayeona moyo wa kila mtu hakika humlipa kwa mema. Ruthu alipotimiza wajibu wake, alifanya hivyo kwa moyo wa kweli na usiobadilika. Tangu alipokuja na mama mkwe wake, hakujuta kamwe kwa uamuzi wake, bali aliendelea kumhudumia kwa moyo uleule aliokuwa nao mwanzoni.
Walipohamia Bethlehemu pamoja na mama mkwe wake, Ruthu alihitaji kutafuta chakula mara moja. Kwa furaha alikusanya masuke yaliyokuwa yameanguka chini na kumhudumia mama mkwe wake kwa chakula hicho. Alijali moyo wa mama mkwe wake, kwa hiyo alimweleza kwa kina kila jambo lililomtokea siku nzima na kumheshimu kwa upendo.
Tendo la Ruthu lilijulikana kwa watu wa Bethlehemu naye akasifiwa. Habari hizo zilimfikia Boazi, mmoja wa viongozi wa kijiji na jamaa wa karibu wa pili aliyestahili kukomboa ardhi ya Naomi. Hatimaye Boazi alimwoa Ruthu, wakamzaa Obedi, aliyekuwa baba yake Yese, baba yake Daudi.
Hivyo, jina lake likaandikwa katika ukoo wa Yesu. Ninaomba kama Ruthu, kila mmoja wenu atimize kwa moyo mwema wajibu wake wote kwa familia na watu wanaomzunguka bila kubadilika, na pia atafute na kufuata njia ipasayo machoni pa Mungu, ili apokee upendo na baraka ambazo Mungu ameandaa. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo!
His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee
Ninaomba maisha yenu yajazwe upendo na baraka za Mungu. Ningependa kushiriki nanyi neema kupitia ujumbe wenye kichwa “Ukarimu wa Wema.”
Ninaomba maisha yenu yajazwe upendo na baraka za Mungu. Ningependa kushiriki nanyi neema kupitia ujumbe wenye kichwa “Moyo wa Kweli.”
Ninaomba maisha yenu yajazwe upendo na baraka za Mungu. Ningependa kushiriki nanyi neema kupitia ujumbe wenye kichwa “Matunda.”