Nina Kiu

Unabii tunaoupata katika Biblia uliandikwa na watu walioongozwa na Roho Mtakatifu, wakinena kutoka kwa Mungu. Kuhusu unabii wa mateso ya Masihi, Zaburi 69:21 inasema, “Walinipa uchungu kuwa chakula changu, nami nilipokuwa na kiu walininywesha siki.” Unabii wa Biblia umetimia kama ulivyonenwa.

Yesu aliponing’inizwa msalabani na kusema, “Nina kiu,” watu walichukua sifongo iliyojaa divai kali, wakaiweka kwenye tawi la hisopo na kuipeleka kinywani mwake. Kwa nini Yesu, Mwana wa Mungu, alisema alikuwa na kiu? Adhabu ya kusulubiwa ilikuwa ya kutisha sana hivi kwamba mtu mwenye mwili aliponing’inizwa msalabani, hangeweza kufanya lolote ila kuvumilia maumivu makali na kiu isiyovumilika.

Hata hivyo, Yesu aliposema, “Nina kiu,” hakumaanisha kiu ya mwili. Maneno hayo yana maana ya kina ya kiroho. Alikuwa amewakomboa wanadamu wote kutoka katika dhambi zao kwa kulipa kwa damu yake; kwa hiyo alitamani kwamba kila anayesikia kilio chake hiki cha dhati azime kiu yake kwa kumlipa kwa ajili ya damu yake.

Ndiyo maana watoto wote wa Mungu wanapaswa kuitikia wajibu wao wanaposikia sauti ya Bwana Yesu akisema, “Nina kiu,” na kumlipa kwa ajili ya damu yake. Tufanye nini hasa ili kulipa gharama aliyolipa? Kwanza kabisa, tunapaswa kuwaongoza kwa Bwana watu wengi wasiomjua Kristo na wanaoishi gizani. Hiyo ni njia ya kulipa gharama ya damu yake, kwa maana Yesu alisulubiwa ili kuwaokoa wale wasioumjua Mungu na ambao wangeangamia jehanamu. Nafsi inapohubiriwa na kuokolewa, Mungu hufurahi sana na atatupa thawabu mbinguni kwa kuihubiria nafsi hiyo.

Pili, tunaweza kulipa gharama ya damu ya Yesu tunapokuza Ufalme wa Mungu kwa kumtolea sadaka kadiri tuwezavyo.

Tatu, maombi yetu ya bidii kwa ajili ya Ufalme na haki ya Mungu yanaweza kuzima kiu yake tunapomlipa kwa ajili ya damu yake. Kupitia maombi ya bidii tunapokea nguvu kutoka juu; kwa nguvu hizo tunaweza kuyaongoza nafsi nyingi kwenye njia ya uzima na kutimiza wajibu tuliopewa na Mungu.

Tumeokolewa kwa upendo wa Mungu Baba na neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Ninaomba kila mmoja wenu amlipe Bwana kwa ajili ya damu yake kwa maombi, kuhubiri Injili na kutoa sadaka mbalimbali. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu! Amina.

   His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee

Word of Life