Amri Kumi – Amri ya Tisa

Kifungu cha Biblia: Kutoka 20:16   
“Usimshuhudie jirani yako uongo.”

Ndugu wapendwa, leo tutaangalia Amri ya Tisa: “Usimshuhudie jirani yako uongo.” Watu wengi hujivunia kutosema uongo, lakini ukweli ni kwamba wengi wetu hudanganya—kwa mambo makubwa na madogo. Kama vile vumbi laini au madoa yasiyoonekana gizani yanavyoonekana kwenye mwanga mkali, mbele za Mungu ambaye ndiye kweli yenyewe watu wengi huonekana wakitoa ushuhuda wa uongo. Nawahimiza mjichunguze kwa Neno kuona kama ndani yenu mna uongo wowote. 

Mtakapokuwa mbele za Mungu, mtambuliwe kuwa watoto wa nuru wasio na uongo wowote. Kwanza, kutoa ushuhuda wa uongo ni kusema jambo lisilo kweli—kudai tendo limefanyika wakati halikufanyika, au kinyume chake. Jambo hili ni zito hasa mahakamani, ambako maneno ya shahidi yanaweza kuathiri moja kwa moja hukumu. Shahidi wa uongo anaweza kumsababishia mtu asiye na hatia hasara kubwa au hata kuhatarisha maisha yake. Mungu anasisitiza kwamba shahidi na wale wanaotoa hukumu wawe waangalifu. 

Kumbukumbu la Torati 19:15 inasema, “Shahidi mmoja asisimame juu ya mtu kwa habari ya uovu wo wote, au kwa habari ya dhambi yo yote, katika dhambi aitendayo; kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.”

   Soma Zaidi     

About the Speaker

President of Manmin World Mission.   - Chairperson of the United Holiness Church of Jesus Christ. 

Rev. Dr. Soolin Lee has been invited in many countries for mission work; including Honduras, Israel, Kenya and Russia. She leads Divine Healing meetings once after every 2 months. Whereby countless people receive healing and answers to their problems; testifying that the bible is true, through various works of the Holy Spirit.

Related Sermon