Amri Kumi – Amri ya Kwanza

Andiko la Biblia la leo: Kutoka 20:1–3
“Mungu akanena maneno haya yote, akasema: Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.”

Ndugu wapendwa, kuna mambo ya msingi unayopaswa kuyajua unapokuwa Mkristo. 

Miongoni mwake ni Sala ya Bwana, Imani ya Mitume na Amri Kumi. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake Sala ya Bwana ili wajue jinsi ya kuomba. Sala hiyo ni mfano wa jinsi Wakristo wanavyopaswa kumwomba Mungu. Imani ya Mitume ni tamko la kawaida la imani ya waumini. Amri Kumi ni msingi muhimu wa kukumbuka, kwa kuwa ndizo amri ambazo Mungu aliwapa Waisraeli kupitia Musa. 

Maneno yote ya Mungu yaliyoandikwa katika vitabu 66 vya Biblia yalifupishwa katika amri kumi, ambazo ni kama nguzo kuu za Biblia. Ingawa haiwezekani kukariri Biblia yote, ni muhimu angalau kuzikariri na kuzitii Amri Kumi kama watoto wa Mungu. Hizi ni desturi za msingi za imani, ndiyo maana katika ubatizo mtu hukiri kwamba atazishika Amri Kumi. 

Hata hivyo, unaweza kuzishika amri vizuri tu unapoelewa maana yake ya kiroho. Kwa mfano, amri ya “Usiue” ina maana ya kiroho iliyo ya kina kuliko kutomuua mtu tu. Wengi wanaweza kufikiri wanaitii kwa kuwa hawajawahi kuua mtu, lakini watatambua sivyo wanapoelewa maana yake ya kiroho. Kupitia mfululizo huu wa mahubiri ya Amri Kumi, naomba mtambue upendo wa Mungu katika kutupa amri zake, mzitie maana zake za kiroho mioyoni mwenu na kuzishika kikamilifu. 

   Soma Zaidi     

About the Speaker

President of Manmin World Mission.   - Chairperson of the United Holiness Church of Jesus Christ. 

Rev. Dr. Soolin Lee has been invited in many countries for mission work; including Honduras, Israel, Kenya and Russia. She leads Divine Healing meetings once after every 2 months. Whereby countless people receive healing and answers to their problems; testifying that the bible is true, through various works of the Holy Spirit.

Related Sermon