Kifungu cha Biblia: Zaburi 37:4
“4 Nawe utajifurahisha kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako.”
Ndugu wapendwa, leo ni Jumapili ya Shukrani, siku ya kumwabudu Mungu kwa shukrani kwa mavuno mengi ambayo Baba Mungu ametubariki nayo mwaka huu. Kwanza tumshukuru na kumtukuza Baba Mungu, aliyetupa baraka kuu rohoni na katika nafsi na kutulinda kwa macho yake yenye kuwaka. Madhabahu ya kanisa imejaa nafaka, matunda na mboga mbalimbali alizotupatia Mungu. Tunatoa shukrani za dhati kwa Huduma ya Wanawake na kwa wote waliofanikisha haya. Tunawashukuru pia wote waliofanya kazi kwa uaminifu na kuzaa matunda mengi kwa ajili ya ufalme wa Mungu. (Mwinjilisti) Tunapotafakari mwaka uliopita, kanisa letu lilipitia nyakati nyingi za kukumbukwa.
Mwaka 2024 tulianza ukurasa mpya nilipoteuliwa kuwa Mchungaji Mkuu. Mambo muhimu yalitia ndani mahubiri na maonyesho ya Pasaka yaliyoheshimu kifo cha kishahidi cha Mchungaji Kichul Ju; Mkutano wa Majira ya Joto wa Manmin uliojaa nguvu; umisionari wa ng’ambo; ziara katika nyumba ya maombi ya Gethsemane; mikutano ya maombi ya Danieli tuliyoahidi kuhudhuria; na mikutano ya uponyaji wa kiungu. Matukio mengine ya kukumbukwa yalikuwa kuzinduliwa kwa Manmin Radio na chaneli ya YouTube ya Bible Only inayopatikana katika lugha 12, pamoja na ibada na sherehe ya maadhimisho ya miaka 42 ya kanisa.
Matukio hayo yenye maana yalifuatana. Mmeomba na kutumikia kwa moyo wenu wote kwa ajili ya kanisa na mimi, ili kudhihirisha utukufu wa Mungu.